У нас вы можете посмотреть бесплатно UTAPELI WA AJIRA FUONI, ZAIDI YA VIJANA 100 WATAPELIWA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Suala la ajira limekuwa ndoto ya kila mwanadamu katika safari ya maisha yake. Kwa maneno rahisi, ajira ni miongoni mwa nyenzo muhimu inayomsaidia mtu kujiendesha kimaisha na kujipatia kipato cha uhakika. Kutokana na umuhimu wake, kila mtu hufanya jitihada mbalimbali kuhakikisha anafikia hatua ya kupata ajira. Mara nyingi wazazi hujitahidi kwa nguvu zote kuwalea na kuwasomesha watoto wao, wakiamini kuwa mwisho wa safari yao ya elimu utazaa matunda ya ajira bora. Na inapofika wakati wa kutafuta kazi, baadhi ya wazazi hutumia kila njia waliyonayo kuhakikisha mwanaye anapata nafasi hiyo muhimu. Hata hivyo, licha ya jitihada zote hizo, bado yapo makundi ya watu wanaoitumia haja hii muhimu ya wananchi kama mwanya wa kuwatapeli na kurejesha nyuma juhudi za wazazi na vijana. Katika harakati za kukuletea taarifa, mtazamaji wa Asam Online TV, leo tumekuandalia mkasa uliozikumba baadhi ya familia hapa Zanzibar, hususan katika eneo la Fuoni Mambo Sasa, ambako kumeripotiwa tukio la utapeli uliowahusu zaidi ya vijana 100. Vijana hao waliombwa kuchangisha fedha kwa ahadi ya kupewa ajira ahadi ambayo haikuwa na uhalisia wowote.