У нас вы можете посмотреть бесплатно MASHUHUDA WASIMULIA CHANZO CHA AJALI YA BASI MWANGA ILIYOUA 7, MAJERUHI WAFIKIA... или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia dereva wa basi la Kampuni ya Mvungi, lililopata ajali na kusababisha vifo vya watu saba na majeruhi 42. Abiria hao walikuwa wakisafiri kutoka Ugweno, Wilaya ya Mwanga, kuelekea jijini Dar es Salaam. Ajali hiyo imetokea leo, Alhamisi, Aprili 3, 2025, saa moja asubuhi, katika eneo la Kikweni, Kijiji cha Mamba, Kata ya Msangeni, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro. Basi walilokuwa wakisafiri abiria liliacha njia na kupinduka kwenye bonde, na kusababisha vifo vya watu hao. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema kuwa wanamshikilia dereva huyo kwa mahojiano zaidi kuhusiana na ajali hiyo. Kamanda Maigwa amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kulimudu gari wakati alipokuwa akipishana na jingine kwenye kona kali, na hivyo kuacha barabara na kutumbukia bondeni. Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi