У нас вы можете посмотреть бесплатно WAJUMBE GEITA MJINI, CHATO KASKAZINI WANASA KWENYE 18 ZA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA RUSHWA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#mwangazatvupdates Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Geita imewakamata baadhi ya wajumbe wa Umoja wa Wanawake (UWT) kutoka kata ya Nyankumbu, jimbo la Geita Mjini na Wajumbe wa Chato Kaskazini kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya rushwa kutoka kwa watia nia wa ubunge. Tukio hili lilitokea tarehe 2 Agosti 2025 baada ya picha za video kuonyesha wajumbe wakigawana fedha kusambaa kwenye mitandao ya kijamii. Kwa mujibu wa taarifa ya TAKUKURU, baada ya tukio hilo kusambaa, ofisi ya mkoa ilichukua hatua ya haraka kwa kuwatambua na kuwakamata wajumbe waliokuwa wakionekana kwenye picha hizo na kwamba Inadaiwa kuwa vitendo hivyo vilifanyika mara baada ya zoezi la kuwanadi wagombea ubunge kukamilika. Katika tukio jingine, tarehe 4 Agosti 2025, TAKUKURU ilipokea taarifa kuwa chakula na vinywaji vilitolewa kwa wajumbe siku ya upigaji kura za maoni katika jimbo la Chato Kaskazini, picha za tukio hilo zilisambazwa pia kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha TAKUKURU kuanza msako na kuwakamata washukiwa kwa ajili ya mahojiano. Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Geita James Ruge, amesema kuwa kutokana na matukio haya na mengine, ofisi imeanzisha uchunguzi unaoelekea kukamilika, ikiwa ni hatua ya kukusanya ushahidi ili kuthibitisha tuhuma za rushwa dhidi ya wahusika.