У нас вы можете посмотреть бесплатно Makala: Mfahamu Oliver Mtukudzi, Sauti ya Afrika iliyookoa mamilioni или скачать в максимальном доступном качестве, которое было загружено на ютуб. Для скачивания выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wingu zito la majonzi lilitanda juu ya anga la Afrika na Dunia kwa ujumla jana majira ya mchana, baada ya kutangazwa kuwa Sauti ya Afrika, Jiwe la Afrika na Gitaa la Haki, Oliver “Tuku” Mtukudzi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 66. Ulikuwa wakati mgumu kwa Zimbabwe ambayo siku zote iliikumbuka sauti ya Oliver Mtukudzi kama alama iliyochagiza kupatikana kwa uhuru wa nchi hiyo kutoka kwenye mikono ya makaburu. Sauti iliyowatetea, iliyowatoa machozi lakini pia iliyowafanya wacheze na kuruka kama ndama. Kwa ujumla alikuwa alama ya muziki wa Zimbabwe iliyokubalika duniani. Alizaliwa September 22 mwaka 1952 katika mji mdogo wa Highfield, jijini Harare nchini Zimbabwe, wakati huo inaitwa Rhodesia. Akiwa miongoni mwa watoto sita wa mzee Mtukudzi, aliishi na kukulia katika mji huo uliokuwa na makazi duni. Alikuwa mtoto mwenye kipaji cha aina yake, aliyebarikiwa na Mungu kuitumia sauti yake kwa ajili ya wanyonge. #RIPMtukudzi #MfahamuMtukudzi -- Dar24 ni chanzo namba moja cha habari kwa watanzania mahali popote walipo duniani. Kwa habari za uhakika kutoka nyanja mbali mbali tembelea www.dar24.com #Dar24 #Dar24Media