У нас вы можете посмотреть бесплатно MAJANGILI SUGU WAWILI WANASWA NA MENO SITA YA TEMBO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Morogoro: Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limeendelea na oparesheni zake maalumu za kuwakamata wahalifu wanaojihusisha na matukio mbalimbali ikiwemo ya ujangili wa wanyama pori pamoja na utapeli wa kimtandao. Katika Wilaya ya Ulanga Julai 14, 2025 wamefanikiwa kumkamata Televaeri Ruben Paranjo (47) na Freddy Maximilian Magumba (42) wote ni wakazi wa Kijiji cha Isongo wilayani humo wakiwa na meno sita ya tembo. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Alex Mkama, wawili hao walikuwa wakisakwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za kujihusisha na uwindaji haramu wa wanyama pori katika Hifadhi za Taifa. Katika hatua nyingine Jeshi hilo la Polisi limekita kambi maalumu wilayani Kilombero kwa lengo la kukabiliana na wahalifu wa utapeli wa kimtandao maarufu 'Halo halo', moja ya sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na ukanda huo kuwa na idadi kubwa ya watu wanaokamatwa kujihusisha na vitendo hivyo. Kwa mujibu wa taarifa za kamanda Mkama kwa vyombo vya habari, Wilaya ya Kilombero inaonesha kuwa na idadi ya watu wengi wanaokamatwa kujihusisha na vitendo hivyo, miongoni mwao ni taarifa aliyoitoa hivi karibuni jumla ya kuwakamata watu 21 katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo Wilaya ya Kilombero, Kilosa na Mvomero, kati yao 21 watuhumiwa 13 wamekamatwa Wilaya ya Kilombero. (Imeandaliwa na Jackson John).