Русские видео

Сейчас в тренде

Иностранные видео




Если кнопки скачивания не загрузились НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru



MAJALIWA USO KWA USO NA TAIFA STARS, AWAPA UJUMBE WA RAIS

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameitembelea Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) inayofanya mazoezi kwenye uwanja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassaan anamatumaini makubwa kuwa timu hiyo itafanya vizuri kwenye michezo yote miwili. Majaliwa ameyasema hayo Oktoba 07, 2024 wakati akizungumza na wachezaji, benchi la ufundi pamoja na viongozi wakiwa katika maandalizi ya michezo miwili ya kufuzu michuano ya AFCON 2025 dhidi ya Congo itakayochezwa Oktoba 10 na 15, 2024. “Kila mmoja aone ana jukumu kubwa, kwako wewe mwenyewe na kwa nchi yako, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia anawatakia kila la kheri na alichofanya ametoa usafiri wa uhakika wa ndege itakayowapeleka nchini Congo kwa ajili ya mchezo wa Oktoba 10, 2024, hili ni jambo kubwa.” Majaliwa amesema kuwa kwa jitihada za Rais Dk. Samia amefanikiwa kushawishi mashirikisho ya mpira wa miguu ya Afrika na FIFA ili kuiona Tanzania ni nchi ambayo imeamua kuboresha viwango vya michezo ikiwemo mpira wa miguu. Follow us on: FACEBOOK; SpotiLeo:   / spotileo-176.  . HabariLeo:   / habarileo   DailyNews:   / dailynewstz   INSTAGRAM; HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig... SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid... TWITTER; Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09

Comments