У нас вы можете посмотреть бесплатно MANARA - HAITATOKEA YANGA AMFUNGE SIMBA MILELE YANGA WANAPASWA WANYWE SUPU KWA KUTOA SARE NA SIMBA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Aliyekuwa Msemaji wa zamani wa klabu za Simba SC na Young Africans SC, ambaye kwa sasa ni Diwani wa Kata ya Kariakoo, Ndugu Haji Manara, amesema kuwa kwa mtazamo wake na kwa yeyote mwenye uelewa wa soka la Tanzania, ni vigumu kuamini kuwa Yanga inaweza kuifunga Simba milele. Manara ametoa kauli hiyo kufuatia mchezo wa Dabi ya Kariakoo uliowakutanisha watani hao wa jadi, akisisitiza kuwa ushindani wa klabu hizo mbili ni wa kihistoria na hauwezi kumpa ubora wa kudumu upande mmoja. “Ni mshabiki mwendawazimu tu atakayeamini kwamba Yanga anatakiwa aifunge Simba milele. Narudia, katika mpira hilo jambo halipo. Kwahiyo sisi (Yanga) leo kupata sare na Simba isichukuliwe kama tumepoteza sana, tungewafunga milele? Hicho kitu hakipo" Alisema Manara. Diwani huyo alitazama mechi hiyo akiwa nchini Afrika Kusini, sambamba na Mtangazaji Oscar Oscar pamoja na mchekeshaji Mpoki, ambapo kila mmoja wao alitoa tathmini yake kuhusu mwenendo wa mchezo huo. Manara alibainisha kuwa licha ya matokeo ya siku hiyo, ushindani kati ya Simba na Yanga utaendelea kuwa na sura tofauti kila wanapokutana. Kwa upande wao, Oscar Oscar na Mpoki walizungumzia ubora wa vikosi, mbinu za makocha pamoja na morali ya wachezaji, wakikubaliana kuwa Dabi ya Kariakoo imeendelea kuwa kivutio kikubwa cha soka la Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.