У нас вы можете посмотреть бесплатно # LIVE : MAOMBI KWA AJILI YA UCHUMI ,BIASHARA NA KAZI-18/21 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
NEW VINE CHURCH MAOMBI YA KUFUNGA YA SIKU 21 MWAKA 2026 SIKU #18 MAOMBI KWA AJILI YA UCHUMI, BIASHARA NA KAZI. OMBI #13. MAOMBI KWA AJILI YA UCHUMI, BIASHARA NA KAZI. "Mbingu ni mali yako, nchi nayo ni mali yako, ulimwengu na vyote viujazavyo Ndiwe uliyeupiga msingi wake." Zab 89:11. "Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi." Hagai 2:8. i. _*"Ni neno jema kumshukuru BWANA,Na kuliimbia jina lako, Ee Uliye juu."*_Zab 92:1. Baba, mbingu na nchi ni mali yako, na vyote viujazavyo. Fedha na dhahabu ni mali yako. nakushukuru mali, fedha dhahabu na uchumi wote uliopitisha mikononi mwangu mwaka jana. ii. "Afichaye dhambi zake hatafanikiwa;Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema." Mithali 28:13 . Baba, kila uovu katika idara yoyote ya kazi zangu, biashara, uchumi, Ee Bwana naomba unisamehe, damu ya Yesu itakase na kuusafisha uchumi wangu na kazi za mikono yangu, ofisi na kila eneo linalohusiana na kipato changu. iii. "Umkabidhi BWANA njia yako, Pia umtumaini, naye atafanya." Zab 37:5. Ee Bwana wewe ndio mmiliki wa vyote kwa hiyo naweka wakfu biashara yangu na kazi za mikono yangu kwako. iv. Naweka wakfu kila kifaa cha uchumi wangu, biashara yangu na kazi za mikono yangu, kwenye mikono yako. v. "Akaenda zake, akaanza kuhubiri katika Dekapoli, ni mambo gani makuu Yesu aliyomtendea; watu wote wakastaajabu." Marko 5:20. Bwana Yesu nitendee mambo makuu katika kazi, biashara, miradi na Uchumi wangu mwaka huu watu wote wastaajabu na kukusifu wewe. vi. "Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana; Mambo ajabu yasiyo na hesabu;" Ayubu 5:9. Ee Mungu, wewe mambo makuu yasiyotambulikana, mambo ya ajabu na yasiyo na hesabu unitendee mambo ya ajabu ya matokeo makuu kwenye kazi zangu, biashara zangu, miradi yangu na uchumi wangu. vii. "Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake; Ni nani afundishaye kama yeye?." Ayubu 36:22. Ee baba unifundishe mwaka huu na kwa uweza wako ukatende makuu katika kazi, biashara, miradi na uchumi wangu. viii. "Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,..." Zab 60:12a. Ee Mungu, Neno lako linasema kwa msaada wa Bwana nitatenda mambo makuu, Ee Bwana ule msaada wako unaosababisha mtu kutenda mambo makuu (kuwa na matokeo makuu), naomba huo msaada ee Jehova, naomba huo msaada ee Yesu juu ya kazi, biashara, miradi na uchumi wangu. Pastor James Kalekwa Resident Pastor New Vine Church - Dodoma +255 754 917 764