У нас вы можете посмотреть бесплатно HESHIMA MNAYONIPA ANASTAHILI MUNGU NA MTEULE WANGU"- RC MAKONDA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
"HESHIMA MNAYONIPA ANASTAHILI #MUNGU NA MTEULE WANGU"- RC #MAKONDA Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amesema yote anayoyafanya Mkoani Arusha yanatokana na utashi, dhamira njema na maelekezo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuhudumiwa wananchi muda wote na kutatuliwa changamoto zao Mbalimbali. Mhe. Makonda ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na maelfu ya wakazi waliojitokeza kwenye siku ya pili ya Kambi maalumu ya Matibabu inayoratibiwa na ofisi yake, akikumbusha kuwa hata heshima anayopewa Mkoani hapa inatokana na Nia njema na Mapenzi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Watanzania. Mh. Makonda ameahidi pia kuendelea kutumia nafasi yake na imani ya Rais Samia kwake, katika kuhakikisha kuwa wananchi wanahudumiwa kikamilifu pamoja na kutatuliwa changamoto mbalimbali hususani za kiafya na kijamii zinazowakabili wakazi wa Arusha. Mhe. Paul Christian Makonda amesisitiza shukrani za zoezi hili kumrudia Mungu na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, akitaka wakazi wa Arusha kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kheri, afya njema na Mungu kumpa maono zaidi katika kuwatumikia wananchi wa Tanzania. Jumanne Juni 25, 2024 imekuwa siku ya pili kati ya siku Saba za Kambi hiyo ya matibabu itakayofikia tamati yake Jumapili wiki hii na Mkuu wa Mkoa ameendelea kukagua huduma zinavyotolewa pamoja na kutoa pole kwa wagonjwa wanaotoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Arusha na nje ya Mkoa wa Arusha kwaajili ya matibabu. #WikiYaAfyaArusha#AfyaKwanza#AfyaBora#TunzaAfyaYako#ArushaHealthWeek#AfyaNiMtaji#FurahaYaAfya#AfyaNjema#ElimuYaAfya#MaishaBora