У нас вы можете посмотреть бесплатно KESI...!! Alichokisema wakili wa 'MFALME ZUMARIDI', baada ya kesi kupigwa kalenda или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Diana Bundala maarufu kama 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 83 leo wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Mwanza kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali katika shauri namba 12/2022 linalowakabili. Kwenye shauri hilo lililosikilizwa katika Kituo Jumuishi cha Utoaji wa Haki kilichopo Busweru wilayani Ilemela mkoani Mwanza mhubiri huyo na wafuasi wake wanashtakiwa kwa kufanya kusanyiko lisilo na kibali na kufanya shambulio la kudhuru mwili kwa maofisa wa Jeshi la Polisi kinyume na kifungu namba 241 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Akisoma maelezo ya awali kwa washtakiwa Wakili wa Serikali Mwandamizi Dorcas Akyoo amesema Zumaridi na wenzake walifanya shambulio la kudhuru mwili dhidi ya askari wa Polisi mwenye namba G1727 James, F5639 Evodius ba Mkaguzi wa Polisi Ntemi Msiri. Akyoo ameiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa walitekeleza shambulio hilo kwa kuwapiga mateke na ngumi katika maeneo mbalimbali ya miili yao na kuwasababishia maumivu. Amesema mbali na kushambuliwa na watu hao, Maofisa wa Jeshi hilo walioambana na kufanikiwa kuwaweka washtakiwa chini ya ulinzi. Baada baada ya kuwaweka chini ya ulinzi maofisa hao waliwachukua washitakiwa na kuwafikisha katika kituo cha Polisi wilaya ya Nyamagana mkoani humo kwa ajili ya mahojiano kisha kufungua kesi dhidi yao ndani ya mahakama hiyo. Upande wa Utetezi katika shauri ukiongozwa na Wakili Msomi, Erick Mutta, Steven Kitale na Anyimike Mwamsiku anayemwakilisha mshtakiwa namba 11 umesema hauna pingamizi kwenye maelezo yakiyosomwa na Jamhuri kwa washtakiwa. Baada ya kusikiliza maelezo ya awali katika kesi hiyo Hakimu, Monica Ndyekobora ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 3 mwaka huu. Katika hatua nyingine shauri la Jinai namba 10/2022 linalomkabili Zumaridi ambalo ni Usafirishaji haramu wa binadamu limeahirishwa hadi Juni 7,2022 kwani mahakama hiyo haina uwezo wa kulisikiliza. Mwisho.