У нас вы можете посмотреть бесплатно RC MRINDOKO ATANGANA OPERESHENI YA SAA 72 USAFI WA MAZINGIRA KATAVI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Hoza Mrindoko, ametangaza operesheni maalum ya saa 72 ya kufanya usafi wa mazingira kwa wananchi wote wa Mkoa wa Katavi, akisisitiza umuhimu wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda afya ya jamii na kutunza mazingira. Ametoa agizo hilo leo Machi 9, 2026 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti uliofanyika ngazi ya Mkoa, akibainisha kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza uhamasishaji wa wananchi katika masuala ya uhifadhi na usafi wa mazingira. Akizungumza katika hafla hiyo, RC Mrindoko amesema mazingira safi ni msingi wa afya bora kwa wananchi na maendeleo ya jamii. “Natoa muda wa saa 72 kwa wananchi wote wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanafanya usafi wa mazingira katika maeneo yao ya makazi na biashara. Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha tunalinda mazingira yetu kwa manufaa ya afya zetu na kizazi kijacho,” amesema Mrindoko. Amesisitiza kuwa suala la usafi wa mazingira halipaswi kuachwa kwa serikali pekee, bali linahitaji ushiriki wa kila mwananchi katika kuhakikisha maeneo wanayoishi yanakuwa safi na salama. Aidha, amewataka wananchi kushirikiana na viongozi wa mitaa na vijiji pamoja na halmashauri katika ukusanyaji na utupaji sahihi wa taka ili kuepusha athari za kiafya zinazoweza kusababishwa na uchafu wa mazingira.