У нас вы можете посмотреть бесплатно Sakata la aliyevunja Kanisa Katoliki Geita bado bichi, aendelea kusota rumande или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kijana Elpidius Edward(22) mkazi wa mtaa wa Katundu wilaya ya Geita anaeshtakiwa kwa makosa mawili ya kuvunja na kuingia kwenye jengo la kanisa na kuharibu mali ya kanisa kuu la Kiaskofu jimbo Katoliki Geita yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 48.2 ameendelea kusota rumande kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya dhamana. Kijana huyo alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Machi 6,2023 na kupewa haki ya dhamana lakini alikosa mdhamini na kurudi rumande hadi jana machi 20 kesi hiyo namba 62/2023 ilipokuja kwa ajili ya kutajwa. Hakimu aliyesikiliza shauri hilo Nyakato Bigirwa alimweleza mtuhumiwa kuwa dhamana iko wazi na kumtaka kuwa na wadhamini wawili watakaokuwa na fedha taslimu Sh24.1milioni au kuwa na hati ya ardhi yenye thamani ya fedha hizo ambapo Wadhamini waliokuwa mahakamani hapo hawakukidhi vigezo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 4,2023 itakapokuja kwa ajili ya kusomewa hoja za awali.