У нас вы можете посмотреть бесплатно SERIKALI KUKOMESHA WAHAMIAJI HARAMU WANAOMILIKISHWA ARDHI KINYUME CHA SHERIA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
SERIKALI KUKOMESHA WAHAMIAJI HARAMU WANAOMILIKISHWA ARDHI KINYUME CHA SHERIA Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amewataka viongozi wa mikoa na wilaya kukomesha tatizo la baadhi ya wahamiaji haramu wanao miliki ardhi kinyume na sheria katika maeneo ya wilaya zilizo mipakani mwa nchi. Waziri Lukuvi ameyasema hayo wakati alipofanya ziara katika Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera wakati wa utekelezaji wa kampeni yake ya ‘Funguka kwa Waziri’ inayowapa fursa wananchi walio na kero za migogoro ya ardhi kuziwasilisha ana kwa ana kwa Waziri wa Ardhi na kupatiwa ufumbuzi papo hapo. “Baadhi ya nyinyi madiwani na viongozi katika mikoa na wilaya za mipakani huku mmekuwa mkitumia ardhi kuwahonga wahamiaji haramu kutoka nchi za jirani ili wawape kura katika uchaguzi” amesema Lukuvi. Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi alibaini kuwepo kwa wahamiaji haramu wanaomiliki ardhi kinyume na sheria katika wilaya ya Kyerwa na Karagwe, kitendo ambacho amekitaja kuwa ni hatari kwa usalama wa nchi na rasimali ardhi. Hata hivyo mara baada ya kubaini udhaifu huo Waziri Lukuvi alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu pamoja na viongozi wengine walio katika mikoa na wilaya za mipakani nchini kuwachunguza kwa makini watu wote wanaoomba kumilikishwa ardhi ili kuwabaini kama ni raia wa Tanzania. Wakati akitoa maagizo hayo Waziri Lukuvi amesema kwamba mtu yeyote ambaye sio raia wa Tanzania haruhusiwi kumiliki ardhi, isipokuwa kwa kupitia taratibu za kituo cha Taifa cha Uwekezaji na kutambulika kama muwekezaji wa kigeni. Waziri Lukuvi anataraji kumaliza na ziara yake wilayani Ngara na Kahama kabla ya kwenda wilaya nyingine kwa ajili ya kuendelea na kampeni ya “Funguka kwa Waziri” yenye lengo la kutatua migogoro ya ardhi katika wilaya zote za Tanzania bara.