У нас вы можете посмотреть бесплатно JINSI AKILI YAKO INAVYOFANYA KAZI || JANWARA KISSELA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Nguvu yako kubwa iko ndani yako mwenyewe. Una uwezo wa kudhibiti mawazo yako, hisia zako na mienendo yako. Vitu hivi vya ndani ndivyo vinavyoamua mwelekeo wa maisha yako. Ukijifunza kuvividhibiti vizuri, kufikia malengo yako kunakuwa ni rahisi kwa sababu unakuwa unaongoza maisha yako kwa makusudi, si kwa bahati. Unapaswa kufahamu jinsi unavyofikiri, unavyohisi na unavyotenda na jinsi mambo haya yanavyoathiri maisha yako ya kila siku. Ili kujitawala, ni muhimu kuelewa jinsi akili inavyofanya kazi. Akili ina mifumo miwili mikuu: mfumo wa mazoea (autopilot system) na mfumo wa makusudi (intentional system). Mfumo wa mazoea huongozwa zaidi na hisia na maamuzi ya haraka. Unategemea sehemu ya ubongo inayosaidia kuchukua maamuzi ya ghafla na ndio unaoamua tabia zako za kila siku bila kufikiria sana. Mfumo wa makusudi huendeshwa na fikra za kina na mantiki. Hufanya kazi kupitia sehemu ya ubongo inayokusaidia kufikiri kwa umakini, kutatua matatizo, kujenga mahusiano bora na kufanya maamuzi sahihi. Mfumo huu unahitaji juhudi za makusudi ili ufanye kazi, lakini unapoutumia, unapata uwezo wa kubadilisha tabia zako, kudhibiti hisia zako na kutengeneza maisha unayotamani. Mpendwa, ni muhimu sana kutambua kuwa ni tabia gani huwa unaifanya bila kufikiri na niwapi unahitaji kujithibiti kwa haraka ili uweze kufanya vyema katika kazi na mambo muhimu katika maisha yako.