У нас вы можете посмотреть бесплатно SAMIA LEGAL AID,YALENGA KUENDELEA KUTOA ELIMU MSAADA KISHERIA WANANCHI WENGI WATATULIWA MIGOGORO YAO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amesema kukutana kwa Wanasheria na Mawakili wa Serikali na kujengewa uelewa wa pamoja katika kutoa msaada wa kisheria kwa wananchi ni utekelezaji wa vitendo wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuweka tabasamu kwa wananchi kwa kuondoa changamoto zao. Mhe. Makalla amebainisha hayo leo Januari 28, 2026 Jijini Arusha wakati akimuwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Juma Homera katika ufunguzi wa mafunzo ya Mawakili wa serikali kuhusu msaada wa kisheria, akieleza pia kuhusu mkakati wa serikali wa kuwatumia Mawakili wake katika kutoa msaada wa kisheria katika masuala yasiyokuwa na mgongano wa maslahi. "Niwasihi sana kutumia weledi wenu katika kuhudumia wananchi na zaidi tujenge utamaduni wa kujitolea kwa wananchi kwani huduma za msaada kisheria ni wito lakini pia yachukulieni kwa uzito mafunzo haya na mtoe maoni yatakayoboresha mfumo wa msaada wa kisheria kwani bado tuna idadi kubwa ya wananchi wenye uhitaji." Amesema Mhe. Makalla. Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Franklin Jasson Rwezimula amesema katika mafunzo hayo ya siku tatu, watajengeana uwezo kuhusu huduma za msaada wa kisheria, utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, ushughulikiaji wa mashauri ya ukatili wa kijinsia pamoja na miiko ya utekelezaji wa majukumu ya wanasheria hao.