У нас вы можете посмотреть бесплатно Makabidhiano ya Ndoo na Ving'amuzi kwa wachakataji wa dagaa или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi na Maliasili za Baharini Zanzibar ZAFIRI imegawa vifaa maalum vya kusarifia dagaa vilivyotengenezwa kwa alumini kwa wachakataji wa dagaa. Akizungumza katika hafla hio Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ZAFIRI Dkt.Zakaria Ali Khamis hatua hiyo ni muhimu sana na inalenga kuboresha mnyororo wa thamani katika sekta ya ukaushaji wa dagaa na usalama wa chakula, kulinda afya ya wananchi na kuongeza ubora wa dagaa wanaozalishwa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Hata hivyo Dr. Zakaria Amesema uvumbuzi wa vifaa hivyo vya alumini ni nyenzo nyepesi, na inayostahimili kutoharibika kwa muda mrefu na salama zaidi kwa matumizi jambo ambalo linalosaidia kuhifadhi ubora wa chakula kwa muda mrefu na kupunguza gharama za utafutaji wa vifaa vipya kila siku. Nae Mtafiti wa Taasisi hio Bimkubwa.......Amesema wameweza kufanya utafiti wa awali kuangalia namna ya kupunguza athari hatarishi za utumiaji wa vifaa vya plastik na mabati katika shughuli hizo na kuweza kutumia Aluminium kwa kuangalia ubora , kudumu kwake na kuangalia changamoto zinazoweza kutokea ili kupata matokeo yatayokwenda kuboresha zaidi sekta hio na kusarifu dagaa kisasa. Nao wasarifu waliopokea vifaa hivyo wameishukuru Taasisi hio pamoja na kuelezea kuwa vifaa vya alumini vitarahisisha kazi yao ya kusarifia dagaa na kupunguza hatari zilizokuwa zikisababishwa na matumizi ya ndoo za plastiki na bati wakati wa kuchemsha dagaa pia itasaidia kuongeza thamani ya dagaa na kuwapatia fursa ya kuuza dagaa wenye ubora mkubwa sokoni.