У нас вы можете посмотреть бесплатно #TBC или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Zaidi ya shilingi bilioni 400 zilizowekezwa na serikali kuboresha Bandari ya Tanga zimeanza kuzaa matunda katika ukusanyaji wa mapato baada ya shehena ya mizigo mipya ikiwemo salfa na kopa kuanza kushushwa kwenye bandari hiyo. Akizunguza wakati wa ziara ya Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Meneja wa Bandari hiyo, Masoud Mrisha amesema bandari hiyo imepiga hatua kubwa kutokana na uwekezaji huo. Kwa upande wao, wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi TASAC wameeleza kuridhishwa na kazi iliyofanywa na serikali kwenye bandari hiyo huku Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Mohamed Salum akiwataka wadau kujitokeza kuwekeza na kutumia bandari hiyo. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Buriani ametoa ombi kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) pamoja TASAC kutenga eneo la kushusha bidhaa za salfa ili zisije kwa bahati mbaya zikachanganyika na bidhaa za chakula.