У нас вы можете посмотреть бесплатно MAKAMU WA RAIS BALOZI DKT NCHIMBI ATAKA WATANZANIA WASIBAGUANE KWA UDINI WALA UKABILA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MAKAMU WA RAIS BALOZI DKT NCHIMBI ATAKA WATANZANIA WASIBAGUANE KWA UDINI WALA UKABILA Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi, amewataka Watanzania kuendelea kudumisha umoja, amani na mshikamano kwa kuepuka vitendo vya ubaguzi wa kidini, kikabila na kikanda. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu na Kikristo kutoka mkoa wa Ruvuma katika hafla ya futari (Iftar) aliyoiandaa nyumbani kwake katika kata ya Mateka, Manispaa ya Songea. Hafla hiyo imewakutanisha waumini wa dini zote mbili waliokutana kwa pamoja kushiriki futari katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan sambamba na kipindi cha Kwaresma kwa Wakristo. Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais Balozi Dkt. Nchimbi amesema kuwa kipindi hiki cha mfungo ni muhimu kwa waumini kumrudia Mungu kwa sala na maombi ili kuendelea kuiombea Tanzania ibaki kuwa nchi yenye umoja, amani na mshikamano. Amesema Watanzania wanapaswa kulinda tunu ya umoja wa kitaifa kwa kuhakikisha hawatoi nafasi kwa vitendo vya ubaguzi wa kidini, kikabila au kikanda ambavyo vinaweza kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Ahmed Abbas Ahmed, akitoa salamu za mkoa huo kwa Makamu wa Rais amesema hali ya usalama katika mkoa wa Ruvuma ni nzuri na wananchi wanaendelea kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu. Ameeleza kuwa wananchi wa mkoa huo wanaendelea kufarijika na kufurahia matunda ya uongozi wa Awamu ya Sita unaoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.