У нас вы можете посмотреть бесплатно BREAKING NEWS: TUME YATANGAZA KUONGEZA SIKU MBILI ZA ZIADA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI MPIGA KURA DA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuongeza siku mbili zaidi za zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Mkoani Dar es Salaam ambapo sasa zoezi hilo litamalizika Machi 25, 2025. Hatua hiyo imetangazwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Machi 23, 2025 kufuatia mwitikio mkubwa wa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao wamejitokeza kwa wingi katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioanza Machi 17 na kutarajiwa kumalizika leo Machi 23, 2025. “Hivyo basi, napenda kuwatangazia wananchi wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuwa, Tume imeongeza siku mbili za uboreshaji wa Daftari kwa tarehe 24 na 25 Machi, 2025 na zoezi litakamilika tarehe 25 Machi, 2025 saa 12:00 jioni,” amesema Jaji Mwambegele. Aidha, Jaji Mwambegele amefafanua kuwa baada ya siku hizo mbili Tume haitaongeza muda zaidi. Amesema wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekuwa na mwitikio mkubwa wa kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao tangu siku ya kwanza ya zoezi hilo Machi 17, 2025 ambapo Tume iliongeza mashine za BVR pamoja na watumishi. “Kutokana na mwitikio mkubwa Tume ilichukua hatua za kuongeza mashine za BVR kits pamoja na watumishi katika maeneo yote yaliyoonekana kuwa na watu wengi na hatua hii imewezesha zoezi kuendelea kwa utulivu katika maeneo yote,” amesema Jaji Mwambegele. Alisema baada ya kuongeza mashine za BVR na watumishi katika maeneo mbalimbali yaliyokuwa na changamoto ya watu wengi iliwezesha kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi na kupunguza kwa kiasi kikubwa misongamano kwenye baadhi ya maeneo. Jaji Mwambegele amesema Tume inawapongeza wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwa mara ya kwanza, kuboresha au kuhamisha taarifa zao na kupata kadi mpya kwa wale ambao kadi zao zimepotea au zimeharibika. Katika hatua nyingine Jaji Mwambegele alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa zoezi hilo halihusishi ubadilishaji wa kadi zilizotolewa 2015 na 2025. Na kwamba kujiandikisha zaidi ya mara moja ni kosa na mtu akibainika anaweza kufungwa, kutozwa faini au vyote viwili yaani kufungwa jela na kutozwa faini.