У нас вы можете посмотреть бесплатно DKT MWIGULU ATOA MAAGIZO KWA WIZARA MBILI KUHUSU BANDARI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
DKT MWIGULU ATOA MAAGIZO KWA WIZARA MBILI KUHUSU BANDARI Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwinyi Nchemba, amewaagiza watendaji wakuu wa Wizara ya Ardhi na Uchukuzi kushirikiana kikamilifu katika utekelezaji wa mpango wa awamu ya pili ya ujenzi wa Bandari ya Tanga, ili kuongeza shughuli za utendaji na kuleta manufaa kwa taifa. Bandari ya Tanga ni miongoni mwa bandari za zamani zaidi nchini na imekuwa na mchango mkubwa katika biashara na usafirishaji wa mizigo kwa ukanda wa Kaskazini mwa Tanzania pamoja na nchi jirani. Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua shughuli za bandari hiyo, Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema kwa sasa Bandari ya Tanga ina eneo dogo linalohitaji upanuzi. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfray Kasekenya, amesema ili Bandari ya Tanga iwe na uwezo wa kupokea mizigo kwa wingi, inapaswa kupanuliwa ili mizigo iingie na kutoka kwa urahisi. Huku Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, naye akizungumzia maendeleo ya bandari hiyo. Mradi wa ujenzi wa gati mpya katika Bandari ya Tanga unatarajiwa kuongeza ajira kwa wananchi wa eneo hilo pamoja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika Mkoa wa Tanga. @ Saidraisa #CloudsDigitalUpadates