У нас вы можете посмотреть бесплатно RC BATILDA AKAGUA UJENZI WA MKWAKWANI PLAZA, AHIMIZA WANATANGA KUCHANGAMKIA FURSA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, leo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Mkwakwani Plaza unaotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), akipongeza kasi ya utekelezaji na ubora wa kazi unaoendelea katika eneo hilo. Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Mhe. Burian amesema mradi huo wa thamani ya shilingi bilioni 8.6 ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati inayochochea ukuaji wa uchumi wa Mkoa wa Tanga. Aidha, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kusukuma mbele maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu na makazi. Amesema Mkwakwani Plaza ni mradi wa kisasa unaojumuisha sehemu za biashara na makazi, na kwamba utakapokamilika utaongeza thamani ya mji wa Tanga pamoja na kutoa fursa zaidi za ajira na uwekezaji kwa wananchi. “Ni jambo la kujivunia kuona kuwa kuanzia ujenzi hadi usimamizi wa mradi huu unafanywa na wataalamu wazawa kupitia shirika letu la nyumba. Hii ni hatua kubwa katika kukuza uwezo wa ndani,” amesema Mhe. Burian. Kwa upande wake, Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Tanga, Mhandisi Musa Patrick, amesema jengo hilo litakuwa na maeneo ya maduka na ofisi za kupangisha katika sehemu ya biashara, huku likiwa na gorofa nne za makazi ambapo yumna za vyumba viwili zitauzwa kwa shilingi milioni 178 na za vyumba vitatu kwa shilingi milioni 240, bei zote zikijumuisha VAT. Naye Msimamizi wa Mradi, Mhandisi Ephraim Msigwa, amesema ujenzi wa mradi huo ulianza Juni 2025 na kwa mujibu wa mkataba unatarajiwa kukamilika Juni 2027. Hata hivyo, kutokana na mahitaji makubwa ya wananchi, jitihada zinafanyika kuhakikisha mradi huo unakamilika ifikapo Agosti 2026. Ameongeza kuwa jumla ya wananchi 189 wamepata ajira kupitia mradi huo, hatua inayochangia kupunguza tatizo la ajira na kuongeza kipato kwa familia nyingi mkoani humo. Mradi wa Mkwakwani Plaza unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Mkoa wa Tanga mara utakapokamilika.