У нас вы можете посмотреть бесплатно WAATHIRIKA WA MVUA NYASA WAPATIWA MSAADA WA MABATI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wananchi wa vijiji vya Lulimba na Tingi vilivyopo Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wamepokea msaada wa mabati 124, migongo pamoja na misumari kufuatia kupoteza makazi yao kutokana na mvua kubwa zilizoambatana na upepo mkali zilizonyesha Januari 6, 2026. Mvua hizo zilisababisha athari kwa jumla ya nyumba 30, ambapo nyumba 22 ziliharibika katika kijiji cha Lulimba na nyumba 8 katika kijiji cha Tingi. Vijiji vyote viwili vipo katika Kata ya Tingi, Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa. Akikabidhi msaada huo katika Ofisi ya Kata ya Tingi, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe Peres Magiri, amesema vifaa hivyo vimepatikana kupitia michango ya wadau mbalimbali walioguswa na maafa hayo. Amesema serikali kwa kushirikiana na wadau itaendelea kuhakikisha wananchi wanaopata madhara ya majanga ya asili wanapatiwa msaada wa haraka ili warejee katika hali yao ya kawaida. Katika hatua nyingine, Mhe. Magiri amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Khalid Khalifa, kwa kutoa fedha zilizowezesha kurekebishwa kwa miundombinu ya shule zilizoharibiwa na mvua hizo. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nyasa ndugu Khalid Khalifa amewaagiza viongozi wa Kata ya Tingi kuhakikisha msaada huo unagawiwa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya waathirika, ili kila kaya iliyoathirika ipate stahiki yake.