У нас вы можете посмотреть бесплатно "VIJANA JITUMENI KATIKA KAZI NA UJASIRIAMALI" или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wafanya biashara wa tende na haluwa wamewataka vijana wa Zanzibar kujitolea kufanya kazi kwa bidii ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku, sambamba na kujiepusha na mienendo mibaya inayoweza kuharibu mustakabali wao. Wito huo umetolewa na Kiongozi wa Wauza Tende na Haluwa, Ndugu Abdallah Salum Suleiman, alipokuwa akielezea msukumo uliompelekea kujiajiri bila kutegemea ajira ya Serikali, katika eneo la Darajani, Wilaya ya Mjini. Amesema biashara ya tende na haluwa imemuwezesha kujipatia kipato halali na kuendesha maisha yake kwa uhakika, akisisitiza kuwa vijana wanapaswa kujituma katika kazi na ujasiriamali ili kujiepusha na ushawishi mbaya unaoweza kujitokeza katika maisha ya kila siku. Kwa upande wake, mfanyabiashara Ndugu Juma Said Rubea amesema kuwepo kwa wafanyabiashara kutoka nje kunawasaidia wajasiriamali wadogo kuongeza ujuzi na kuboresha biashara zao, hatua itakayochangia kuimarika kwa soko la tende nchini. Naye Ndugu Ali Khamis Ali ameomba mamlaka husika kuwajengea wajasiriamali wa tende na haluwa maeneo maalumu yenye miundombinu rafiki, ikiwemo mahema, ili kuongeza ufanisi na kuendesha biashara zao kwa weledi na mazingira bora.