У нас вы можете посмотреть бесплатно HAKUNA MTOTO ANAYEACHWA NYUMA: VIONGOZI KWAHANI WAGAWA VIFAA VYA SKULI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kauli isemayo “hakuna mtoto anayeachwa nyuma, kila mmoja anastahili fursa” imeendelea kupewa uhai Jimbo la Kwahani, Wilaya ya Mjini, Unguja Zanzibar, ambapo Mbunge na Mwakilishi wa jimbo hilo wamefika kugawa vifaa vya skuli kwa watoto wenye uhitaji maalum, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora bila vikwazo. Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani, Ndugu Mohammed Sijamini Mohamed, amesema zoezi hilo si ahadi pekee bali ni wajibu na utaratibu wa lazima katika kuwatumikia wananchi na kuimarisha sekta ya elimu jimboni humo. Naye Diwani mteule Nasir Ali Mmanga pamoja na Diwani wa Wadi ya Kwahani, Lutfia Juma, wamesema ugawaji wa sare na vifaa vya skuli ni utaratibu wa kila mwaka unaofanyika mwanzoni mwa mwezi Januari kwa lengo la kuwawezesha watoto kuanza masomo kwa wakati. Kwa upande wao, wazazi na walezi wa watoto hao wameonesha furaha na kutoa shukrani kwa viongozi hao, wakisema hatua hiyo imepunguza mzigo wa gharama za maandalizi ya skuli. Aidha, wameomba zoezi hilo liendelee kuwahusisha watoto wa madarasa yote na si darasa la kwanza pekee. Hatua hii ni muendelezo wa juhudi za kijamii zinazolenga kuhakikisha elimu kwa wote na kuthibitisha kuwa kweli hakuna mtoto anayebaki nyuma. #AsamOnlineTV #ElimuKwaWote #Kwahani #HakunaMtotoAnayeachwaNyuma #ViongoziKwaJamii #Zanzibar