У нас вы можете посмотреть бесплатно 📌Wenye Ulemavu Wang'ara Kilimanjaro. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Jamii ya watu wenye Ulemavu Nchini Imekumbushwa Kuwa ni wao ni wenye thamani na Umuhimu Mkubwa Mbele ya Mungu na Wanadamu hivyo hawapaswi kukata tamaa bali wawe imara na watimize Ndoto zao kadri ya Mapenzi ya Mungu. Mkuu wa Taasisi ya New Life Foundation Askofu Glorious Shoo Amesema hayo Feb 13,2026 wakati wa Hafla Maalum Kwa jina la 'Night to shine' iliyokuwa na lengo la kupeana Zawadi,kula pamoja na Kuzungumza na Watu wenye Ulemavu Mkoani Kilimanjaro. Akizungumza Katika Hafla Iliyowaleta Pamoja Wenye ulemavu pamoja na wageni mbalimbali kutoka Ndani na Nje ya Nchi,Askofu Shoo Amesema sio tu kwamba taasisi hiyo inawasherehekea wenye ulemavu bali inawathamini sana na inatambua mchango wao. Wakizungumza kando ya Mkutano Huo,Mariam Stefano,Chausiku Mkuya, Wamesema hafla hiyo imewakumbusha kujikubali,kujipenda na kujithamini lakini imekuwa nafasi muhimu kwao kukutana na kubadilishana mawazo. insert wenye ulemavu Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wenye UlemavuTanzania(CHAWATA)mkoa wa Kilimanjaro Selestine Mbawala,ameisihi Serikali Kutatua changamoto ya Utolewaji wa Mikopo ya 10% inayomtaka mwenye ulemavu kuwa na biashara ya mfano kabla hajapatiwa mkopo.