У нас вы можете посмотреть бесплатно Dengue ijumuishwe na Malaria kwenye udhibiti? Tazama haya majibu ya watafiti wa Tanzania. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kwa miaka mingi, homa ya dengue, ambayo huenezwa na mbu, imekuwa ikidhibitiwa kwa mipango ya muda mfupi nchini Tanzania. Hatua zinachukuliwa tu wakati wa milipuko. Hata hivyo, malaria, ambayo pia huenezwa na mbu, imekuwa ikishughulikiwa kwa mipango ya muda mrefu na iliyo imara. Katika utafiti mpya, watafiti nchini Tanzania wamependekeza kuwa hatua za kudhibiti dengue zijumuishwe kwenye mipango na programu za kitaifa za kudhibiti malaria. Tunazungumza na Dkt. Nathanael Sirili, kutoka Chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili(MUHAS) ili kupata undani wa utafiti huu uliochapishwa Machi 2024 katika Jarida la Kitabibu la Tanzania, yaani Tanzania Medical Journal (TMJ) ukionyesha umuhimu wa dengue kujumuishwa katika programu zilizopo kama vile za udhibiti wa malaria. Ili kupata taarifa za utafiti mara tu zinapo chapishwa, jisajiri uwe mdau kupitia link hii: https://utafiti.tz/stakeholder/ Kama wewe ni mwandishi wa habari au mtaalamu wa mawasiliano jisajiri kupitia link hii: https://utafiti.tz/journalist-communi...