У нас вы можете посмотреть бесплатно NAIBU WAZIRI ASIMAMISHA WATUMISHI SITA KILOLO KWA TUHUMA ZA UBADHILIFU WA SHULE YA WASICHANA LUGALO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Reuben Kwagilwa, amewasimamisha kazi watumishi sita wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kufuatia tuhuma za ubadhilifu katika mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Lugalo. Awali, Mkuu wa Shule ya Wasichana Lugalo, Naja Msokwa, alisema shule hiyo iliyopo Kata ya Lugalo, Kijiji cha Mbigili, ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 960 kutoka kidato cha kwanza hadi cha sita. Kwa sasa ina wanafunzi 351, wakiwemo 125 wa kidato cha kwanza na 226 wa kidato cha tano na sita katika michepuo ya PCM na PCB. “Lengo kuu la mradi huu ni kuongeza fursa za masomo ya sayansi kwa wasichana,” alisema Msokwa. Hadi sasa ujenzi wa miundombinu umegharimu Sh4.7 bilioni, ambapo Sh4.45 bilioni zimetolewa na Serikali Kuu na Sh250 milioni kutoka mapato ya ndani ya halmashauri. Msokwa alibainisha kuwa mradi huo umekumbwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo ongezeko la gharama na jiolojia ya eneo la ujenzi kuwa tepetevu, hali iliyohitaji misingi mirefu kuliko ilivyokadiriwa kwenye BOQ ya TAMISEMI. Mradi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Lugalo ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Sita, ikilenga kuongeza fursa za elimu kwa wasichana na kupunguza changamoto za masafa mkoani Iringa. Akizungumza leo wakati wa ziara yake wilayani Kilolo, Kwagilwa alisema tathmini ya awali imebainisha kasoro kubwa katika usimamizi wa fedha na utekelezaji wa mradi huo muhimu wa elimu, hatua iliyolazimu Serikali kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliotajwa. “Taarifa zinaonyesha kuwa Wilaya ya Kilolo inasuasua kwenye utekelezaji wa miradi, hususan ya elimu na afya. Leo sijapata nafasi ya kukagua miradi ya afya, lakini nimekagua mradi huu wa sekondari,” alisema.