У нас вы можете посмотреть бесплатно LAMATA: SIJAWAHI KUMUONA MWANAMKE MSAFI KUMZIDI KAJALA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Lamata Mwendamseke, anayejulikana pia kama 'Lamata Leah', ni mwongozaji na mtayarishaji wa filamu nchini Tanzania. Akiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika tasnia, ameshiriki katika utayarishaji wa filamu zaidi ya 40, ikiwemo Kigodoro, Gumzo, Figo, Majuto, Shaymaa, Nesi Selena, Stella, After Death, My Princess, Tikisa, Mr & Mrs Sajuki na Poor Minds. Aidha, amehusika katika uongozi wa tamthilia maarufu kama Kapuni na Jua Kali. Kwa sasa, filamu zake mpya 'Jacob’s Daughter' na 'Nafsi Yangu' zinafanya vizuri sokoni. Lamata anaeleza kuwa changamoto kubwa inayowakumba watayarishaji wa filamu wa kike nchini ni hofu pamoja na kukatishwa tamaa. "Nimeamua kupambana ili kutambulisha watayarishaji na waongozaji wa kike zaidi. Naamini kupitia mimi, wengi watajitokeza," amesema Lamata. Akizungumzia urafiki wake na Kajala, Lamata amesema kuwa walifahamiana kati ya mwaka 2013 na 2014 baada ya Kajala kutoka gerezani. Uhusiano wao ulikuwa kupitia kazi, huku mwigizaji Wolper akichangia kuwaunganisha. "Kajala ni msafi kupita kiasi, sijawahi kukutana na mwanamke anayemzidi katika usafi. Mpaka sasa bado natafuta mtu anayefikia viwango vyake," amesema Lamata. Video na Khatibu Mgeja.