У нас вы можете посмотреть бесплатно Mafunzo ya Zao la Nazi Yafungwa, Ushirikiano Mpya Wawekwa или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Naibu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Dkt. Salum Soud Hamed, amesema Wizara ya Kilimo imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kuwapatia wakulima elimu yenye lengo la kuongeza uzalishaji wa zao la nazi pamoja na mazao mengine nchini . Dkt. Salum ameyasema hayo katika hafla ya kufunga mafunzo ya siku 19 ya Uboreshaji wa Aina za Nazi pamoja na Udhibiti wa Wadudu na Magonjwa ya Mimea, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi. Mafunzo hayo yaliwalenga wataalamu wa kilimo pamoja na wakulima kutoka Unguja na Pemba. Naibu Waziri amesisitiza kuwa uwepo wa Taasisi ya Chinese Academy of Tropical Agricultural Sciences (CATAS) utasaidia kwa kiasi kikubwa kubuni na kutumia njia bora zitakazoongeza uzalishaji wa zao la nazi Unguja na Pemba, kutokana na uzoefu mkubwa wa taasisi hiyo katika masuala ya teknolojia na ubunifu wa kilimo. Aidha, amehimiza ushirikiano ulioanzishwa kati ya CATAS na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo Zanzibar (ZARILI) kupitia hati ya makubaliano kuwa endelevu, ili tafiti zitakazofanywa ziweze kuleta tija katika sekta ya kilimo na kwa jamii kwa ujumla. Awali, akitoa taarifa ya mafunzo hayo, Msimamizi na Mratibu wa Mafunzo kwa upande wa Zanzibar, Bw. Masoud Salum Abdi, amesema Taasisi ya CATAS imefurahishwa na namna washiriki walivyopokea mafunzo kwa uelewa mzuri, na kuahidi kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha teknolojia za kilimo zinawafikia wakulima na kuongeza tija katika uzalishaji. Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Masuala ya Usindikaji kutoka CATAS, Bi. Chen Jiaying, amesema wako tayari kuunganisha utaalamu katika masuala ya uzalishaji na usindikaji wa mazao ili kupata bidhaa bora za kilimo. Ameongeza kuwa taasisi hiyo itajikita zaidi katika mazao ya kijamii yakiwemo nazi, machungwa, maembe na mbogamboga, kwa lengo la kuimarisha mnyororo wa thamani na kuwekeza zaidi katika tafiti zitakazotoa matokeo chanya na yenye manufaa. Naye Bw. Ali Ussi Mohamed, akitoa shukrani kwa niaba ya washiriki wa mafunzo, amesema wanaishukuru Wizara ya Kilimo pamoja na CATAS kwa mafunzo waliyopewa, na kuahidi kuyatumia kwa vitendo ili kuongeza uzalishaji wa zao la nazi pamoja na mazao mengine. Katika hafla hiyo pia, kuliwekwa saini hati ya makubaliano kati ya Taasisi ya Chinese Academy of Tropical Agricultural Sciences (CATAS) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo na Mifugo Zanzibar (ZARILI), kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kufufua kiwanda kilichopo katika Kituo cha Kilimo Bambi, ambacho kilianzishwa kwa ajili ya kuendeleza zao la nazi pamoja na usindikaji wa mazao mengine ya mboga na matunda.