У нас вы можете посмотреть бесплатно MWANAFUNZI FATUMA ISMAIL AOMBA MSAADA ILI KUENDELEA NA MASOMO YA KIDATO CHA TANO. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwanafunzi Fatuma Ismail, mkazi wa Kata ya Chikongola, Manispaa ya Mtwara Mikindani, anaomba msaada wa kuchangiwa ada na mahitaji ya shule ili kuendelea na masomo ya kidato cha tano katika shule ya sekondari Ilulu, mkoani Lindi. Fatuma, aliyemaliza kidato cha nne mwaka 2024 katika shule ya sekondari Umoja, alichaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu. Hata hivyo, kutokana na changamoto za kifamilia na hali duni ya kiuchumi, ameshindwa kuanza masomo kama wenzake waliorejea shuleni Julai 6, 2025. Akizungumza na Mtwara Online Tv, Fatuma amesema anaishi na shangazi yake ambaye ni mlezi wake pekee, lakini kutokana na ulemavu wa miguu hana uwezo wa kumsaidia kifedha. Baba yake alishafariki dunia na hivyo hana msaada mwingine. Mahitaji anayoyahitaji ili kujiunga na masomo ni pamoja na ada ya shilingi 70,000, sare ya shule, tranka, godoro, nauli, madaftari pamoja na vifaa vingine vya kimsichana. Shule inatarajiwa kufunguliwa rasmi Septemba 15, 2025, na anahitaji msaada wa haraka ili kuweza kuripoti kwa wakati. Mtwara Online Tv inawaomba watanzania, serikali pamoja na wadau mbalimbali kujitokeza kumsaidia Fatuma ili kutimiza ndoto zake za kimasomo.Msaada unaweza kutumwa kupitia namba ya simu 0681172234 kwa jina la Fatuma Mmalala.