У нас вы можете посмотреть бесплатно AKATWE MILIONI MBILI KILA SIKU ASITUCHEZEE- RC MHITA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita ameonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara za ndani katika Manispaa ya Kahama na kuagiza hatua kali zichukuliwe dhidi ya mkandarasi anayetekeleza mradi huo, Kampuni ya Sichuan Road and Bridge Group (SRBG). Akiwa kwenye ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo unaotekelezwa kupitia Mradi wa TACTIC iliyofanyika Septemba 30,2025 RC Mhita amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Masoud Kibetu kuandika barua rasmi kwa mkandarasi huyo, ikiambatana na adhabu ya kukatwa milioni 2 kwa kila siku kuanzia Oktoba 1, 2025, baada ya mkataba wake kufikia ukomo tarehe 30 Septemba 2025, bila kazi kukamilika. “Mkandarasi huyu amelipwa zaidi ya shilingi bilioni 5, lakini kasi ya utekelezaji ni ya kusuasua licha ya kuongezewa muda mara mbili. Serikali haina tena sababu ya kumuongezea mkataba,” alisema Mhita kwa msisitizo. Amesema Serikali ya Mkoa haitavumilia kuona fedha za umma zinatumika bila matokeo halisi, akisisitiza kuwa kila mkandarasi anapaswa kuzingatia muda wa utekelezaji na thamani ya fedha inayotolewa kwa miradi ya maendeleo. Katika maagizo yake, Mhita amesisitiza kuwa adhabu hiyo ya kisheria inalenga kulinda maslahi ya wananchi ambao wanasubiri huduma bora za miundombinu na kuonya kuwa hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa endapo mkandarasi atashindwa kumaliza kazi hiyo kwa haraka. Ziara hiyo imekuwa sehemu ya msukumo wa kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakwenda kwa kasi inayostahili, huku RC Mhita akisisitiza uwajibikaji kwa watendaji wote na wadau wa ujenzi katika Mkoa wa Shinyanga Nao baadhi ya wananchi waliokuwepo kwenye mradi huo walimpongeza RC Mhita kwa hatua alizochukua na kumuomba kumsimamia kwa ukaribu mkandarasi huyo katika kipindi ambacho Mvua zinatarajia kunyesha ili wasipate madhara yakiwemo mafuriko kutokana na kutokamilika kwa miundombinu katika manispaa ya Kahama.