У нас вы можете посмотреть бесплатно #LIVE или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#ikulu #ikuluzanzibar #raissamia #uvccmmwanza #rsmwanza #rcmwanza #wazirimkuu #ofisiyamakamuwarais #ofisiyawazirimkuu #bungelatanzania #tamisemi #dodomakwanza #dodomajiji #wizarayamamboyandani #wizarayaelimu MAHAKAMA KUU YAMUAMURU MBUNGE WAITARA KULIPA FIDIA YA SHILINGI BILIONI SITA Jopo la Majaji Watatu wa Mahakama ya Rufani Tanzania leo Jumatatu Februari 23,2026 wameketi Jijini Mwanza kupitia Shauri la Rufaa ya Madai Na.1557/2025 lililowasilishwa na warufani watatu akiwemo Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara walioamriwa na Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Musoma kumlipa fidia ya Sh. Bilioni 6 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Eliakimu Maswi, aliyedai kudhalilishwa na kuvunjiwa heshima yake katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Tarime mkoani Mara. Warufani wengine katika shauri hilo la madai ni Karoli Jacob Karoli na Mara TV, ambao kwa pamoja wanatetewa na wakili Hekima Mwasipu, huku mjibu rufaa Eliakimu Maswi akiwakilishwa na mawakili wawili Makubi Kunju na Kassim Gilla. Juni 16, 2025 Jaji Komba wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Musoma aliwaamuru Waitara na wenzake kumlipa Eliakimu Maswi fidia ya Sh.Bilioni 6, maamuzi ambayo warufani hao waliyakatia rufaa iliyosajiliwa Agosti, 2025 katika Mahakama ya Rufani Tanzania. Jopo la Majaji wa Mahakama ya Rufani wanaopitia marejeo ya rufaa hiyo ya madai katika kikao chao kinachoendelea katika Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Mwanza ni Jaji Levira, Fikirini na Issa.