У нас вы можете посмотреть бесплатно EPISODE 28 ( 19/2/2026 ) : PATACHIMBIKA TUNDU LISSU AMUANIKA VIBAYA SHAHIDI BODABODA KUTOKA MBEYA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
LIVE UPDATES MOJA KWA MOJA KUTOKA MAHAKAMANI EPISODE YA 28 KESI YA UBAINI INAYOMKABILI MWENYEKITI WA CHADEMA MH TUNDU LISSU Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu imeendelea tena leo, Alhamisi Februari 19, 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam ambapo mashahidi mbalimbali wa Jamhuri wameendelea kutoa ushahidi wao Mahakamani hapo. Kesi hiyo Na. 19605/2025 inayosikilizwa mfululizo mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru, awali imeshuhudiwa Mahakamani hapo Askari Polisi mpelelezi H. 937 Detective Koplo Vicent akitoa ushahidi wake, akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Ignas Mwinuka. Shahidi wa pili (2) kwa siku ya leo kutoa ushahidi wake, ambaye ni shahidi wa 13 kwa ujumla wake katika muendelezo wa mashahidi wa Jamhuri ni shahidi wa siri (P3), shahidi huyu ametoa ushahidi wake akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Ajuwaye Nzengeli. Akiwa chini ya kiapo kama ilivyo ada, P3 ameieleza Mahakama kuwa yeye ana umri wa miaka 35, Dini yake ni Muislamu, na kwa takribani miaka minane (8) sasa amekuwa akijishughulisha na uendeshaji wa Bodaboda. Shahidi huyu ambaye ameieleza Mahakama kuwa ni Mkazi wa Mtaa wa Mtengule, Halmashauri ya Jiji la Mbeya, amesema yeye ni mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuanzia mwaka 2021 mpaka sasa, na kwa muda wote huo amekuwa akishiriki kikamilifu matukio na shughuli mbalimbali za chama hicho zinazofanyika mkoani Mbeya. Anasema anakumbuka mwaka 2024 alishiriki kwenye maandamano ya CHADEMA yaliyofanyika Mbeya, ambapo yeye alishiriki kwenye msafara wa maandamano uliioongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa wa wakati huo Freeman Mbowe. Tukio lingine analokumbuka linalohusiana na CHADEMA ni kongamano lililoandaliwa la vijana (BAVICHA) lililopaswa kufanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Ruanda-Nzovwe, lakini kwa bahati mbaya kwao kongamano hilo halikufanyika kwa sababu serikali ililizuia. Huu ni ushahidi ambao fatilia mwamzo mwisho updates hii hapa uhuru online media kuelewa kilichotokea mahakamani leo. #mahakamani #tundulissu #chadema