У нас вы можете посмотреть бесплатно EPISODE 27 ( 19/2/2026): MAJIBIZANO MAKALI LISSU NA KATUGA " SHAHIDI AFANDE HAJUI KIINGEREZA " AIBU или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kesi ya uhaini Na. 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, imeendelea leo Alhamisi, Februari 19, 2026. Shauri hilo linasikilizwa na kazi ya majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru. Leo mahakama imepokea ushahidi kutoka kwa upande wa Jamhuri, ambapo shahidi wa 12 ni H. 937 Detective Koplo Vicent . Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Ignas Mwinuka, shahidi huyo ametoa maelezo yake ya awali kama vile: Wasifu wa Shahidi Umri: Miaka 36. Kituo cha Kazi: Police Central, Mbeya. Elimu ya Jeshi: Alihitimu mafunzo ya awali ya upolisi CCP Moshi, Machi 03, 2012. Majukumu: Kupeleleza kesi, kukamata watuhumiwa, na kutoa ushahidi mahakamani. Maelezo ya Tukio Shahidi ameieleza mahakama kuwa mnamo Aprili 05, 2025 , akiwa katika Kituo cha Polisi Mwanjelwa, alipewa maelekezo na Mkuu wa Kituo kumtafuta mtu aliyetambulika kwa jina la 'P9' . Koplo Vicent amedai kuwasoma na taarifa za siri (fiche) zilizofika kituoni hapo zikimtuhumu 'P9' kufanya uhamasishaji kwenye vijiwe mbalimbali, akichochea kuzuia kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Katika kutekeleza jukumu hilo, shahidi alipewa namba ya simu ya mtuhumiwa huyo, ambaye Mkuu wa Kituo aliipata kutoka kwa taarifa yake (msiri). (Fuatilia undani wa kesi hii kupitia Uhuru Online Media updates moja kwa moja kutoka mahakamani) #mahakamani #tundulissu #chadema