У нас вы можете посмотреть бесплатно WANAWAKE WA MSOMERA WACHACHAMAA, WATAKA KUWA KAMA WAMAMA WA JAMII NYINGINE или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
HANDENI Imeelezwa kuwa ili wanandoa waweze kuepukana na ukatili unaosababishwa na umasikini, wanapaswa kushikamana na kushirikiana ili waweze kuongeza pato la familia, hali itakayochochea amani ndani ya nyumba zao. Hayo yameelezwa na mtaalam wa ujasiriamali kutoka shirika la tree of hope Bi.Agnes Yohana, alipokuwa kwenye semina ya kuvijengea uwezo wa elimu ya fedha na ujasiriamali vikundi vya wanawake wa kijiji cha Msomera wilayani Handeni. Washiriki wa semina hiyo akiwemo Victoria Huho amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuinuka kiuchumi, huku Bi.Upendo Robert akisema elimu waliyoipata imewasaidia kupata ujasiri wa kukopa mikopo ya halmashauri, na Bi. Anjelista Saitot Laizer akisema wanakwenda kuimarisha vikundi vyao ili wamama wa Msomera wawe kama wa maeneo mengine Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii kata ya Misima Bw.Baraka Manoko Maiga amesema katika kukabiliana na mfumo dume, serikali kwa kushirikiana na wadau wakiwemo Tree of Hope wametoa elimu kwa jamii na sasa watu wote wana fursa sawa. Semina hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa Kupinga ukatili wa kijinsia na kujenga ustahimilivu wa jamii katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambao unatekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la tree of hope chini ya ufadhili wa Women fund Tanzania-Trust