У нас вы можете посмотреть бесплатно VIJANA ACHENI MIHEMKO YA MAANDAMANO KAPIGENI KURA-AFANDE SELE или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwanamuziki na mfalme wa mashairi Tanzania, Selemani Msindi maarufu kama Afande Sele,amewataka Watanzania hususan vijana kuacha kuwa na mihemko ya kususia kushiriki Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa kutoshiriki ni kujinyima haki ya kikatiba. Akizungumza na JAMBO TV leo Oktoba 14, 2025, akiwa mkoani Morogoro, Afande Sele amesema vijana wanapaswa kutumia nguvu yao kwa kushiriki katika kupiga kura badala ya kujiingiza kwenye maandamano yanayoandaliwa na watu wasiolitakia mema taifa. Ameongeza kuwa ni muhimu kwa Watanzania kuchagua viongozi wanaojali maendeleo na amani ya nchi, badala ya kufuata ushawishi wa watu wanaopandikiza chuki mitandaoni wakiwa nje ya mipaka ya Tanzania. Afande Sele amehitimisha kwa kusisitiza kuwa uchaguzi ni njia halali ya kuleta mabadiliko, na kila kijana anapaswa kutimiza wajibu wake wa kikatiba kwa kupiga kura.