У нас вы можете посмотреть бесплатно MAZAO YA KIMKAKATI SULUHU YA UHARIBIFU VYANZO VYA MAJI -DKT MUSSA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu pamoja na watendaji wa Bodi ya Saba wametakiwa kuwa na mawazo mbadala yatakayowawezesha wakulima kulima mazao ya kimkakati, ili kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na wananchi wanaoishi pembezoni mwa vyanzo vya maji. Wito huo umetolewa leo, Oktoba 16, 2025, na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Mussa Ali Mussa, wakati wa uzinduzi rasmi wa Bodi ya Saba ya Bonde la Wami Ruvu, uliofanyika mkoani Morogoro. Dkt. Musa amesisitiza kuwa ni muhimu kwa watendaji wa bodi hiyo kuzingatia sheria na taratibu walizoweka ili kufanikisha mabadiliko chanya ya kiuchumi kupitia sekta ya maji. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Elibariki Mmassy, amesema kuwa bodi hiyo imeendelea kutekeleza jukumu lake la kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayosimamia sekta hiyo. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji, Robert Sunday, ameweka bayana kuwa dira ya Dunia na Taifa inalenga kuhakikisha uhakika na usalama wa maji kwa wananchi unaimarika kuanzia mwaka 2025 hadi 2050. Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Saba ya Bonde la Wami Ruvu, Nickson Lutenda, ameainisha mafanikio ya Bodi ya Sita na kueleza mikakati ya kuendeleza mafanikio hayo, hususan katika maeneo ya ukusanyaji wa mapato na namna ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya bodi hiyo.