У нас вы можете посмотреть бесплатно BILIONI 9 KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI LUKOBE, MKUNDI NA KIHONDA – MORO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Zaidi ya Shilingi Bilioni 9 zimetumika kutekeleza miradi ya maji inayolenga kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa kata za Lukobe, Mkundi na Kihonda katika Manispaa ya Morogoro,Kata hizo zimekuwa zikikumbwa na tatizo la ukosefu wa maji kwa muda mrefu, hali iliyosababisha usumbufu kwa wananchi katika shughuli zao za kila siku. Akizungumza kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo, Mkurugenzi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA), CPA Sais Kyejo amesema kuwa mradi huo ni sehemu ya mkakati wa mamlaka hiyo kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa kiwango cha kutosha kwa wananchi wote wa Manispaa ya Morogoro. Kyejo ameeleza kuwa, miradi hiyo inatarajiwa kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji hadi kufikia asilimia 85 katika kata hizo, hatua itakayosaidia kuondoa adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji, hasa kwa wanawake na watoto. Aidha, ameongeza kuwa katika kata za Mindu na Kingolwira pia miradi ya maji inaendelea kutekelezwa, ambapo wananchi wa maeneo hayo nao watanufaika na huduma hiyo muhimu ya maji mara baada ya kukamilika kwa miradi hiyo. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Mussa Kilakala ametoa wito kwa MORUWASA kuhakikisha inasimamia kikamilifu wakandarasi wanaotekeleza miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa,amesisitiza kuwa Serikali haitamvumilia mkandarasi yeyote atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo. Kilakala pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa watendaji wa miradi hiyo, ikiwa ni pamoja na kulinda miundombinu ya maji na kutoa taarifa mapema pindi wanapoona changamoto yoyote inayoweza kuathiri utekelezaji wa mradi.