У нас вы можете посмотреть бесплатно IBARA YA KWANZA YA KATIBA: KUTANGAZA JAMHURI YA MUUNGANO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
IBARA YA KWANZA YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUTANGAZA JAMHURI YA MUUNGANO “Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano” Kwahiyo sasa katiba inasema Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya muungano. Kivipi sasa na muungano upi, ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo kwa kirefu ni Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Haya mataifa au hizi nchi ziliungana rasmi mnamo mwaka 1964 mwezi wa 4 tarehe 26 (ndo maana kila mwaka terehe hiyo na mwezi huo hua tunasheherekea sikukuu ya muungano) na ikawa inaitwa jamhuri ya muungano wa Tanganyika na watu wa Zanzibar baadae sasa tukapata jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ambapo tarehe 22 ya mwezi huo, ilitiwa Saini hati ya muungano hiyo na wahusika ambao ni J.k. Nyerere na A.A. karume, hawa walikua mashuhuda , ambapo tarehe 26 ikapelekwa bungeni kujadiliwa na terehe 27 wakasherehekea muungano huo na kukabidhiana hati za muungano baina ya hizi nchi au mataifa haya. Ambapo sasa tarehe 28 oktoba tukapata jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania na ambambalo mpaka sasa tunalitumia. Sasa unaweza kujiuliza kwa jinsi nilivyoelezea kwa uchache hivi, umesikia neno Tanzania bara ni nini au Tanzania visiwani ni nini au Tanzania Zanzibar nini? Jibu Hapana, maana yake kwenye historia kama nilivyosema awali hakuna neno Tanzania bara, Tanzania visiwani wala Tanzania Zanzibar na kwa maana hiyo hayo maneno hayatambuliki kisheria ila yanatumika tuuh kuelezea eneo husika lakini sio kwa usahihi. Tunajua nchi mbili ziliungana Tanganyika na Zanzibar, kwani tukitumia haya majina tunamaanishi ni nchi mbili? Jibu Hapana, sasa kuna ubaya gani kutumia majina hayo ambayo ukisema tuuh mtu anaelewa kwa urahisi kabisa. Na pia tunatambua kama Katiba ilivyosema kuwa nchi ni moja, kwahiyo Zanzibar sio nchi na Tanganyika sio nchi pia. Lakini ukienda kwenye hati ya muungano inakwambia vizuri mno na kuelezea kuwa nchi moja ila ina serikali mbili au mifumo miwili na mambo ya muungano na yasiyo ya muungano na kwa mujibu wa Katiba, mpaka sasa tuna mambo ya muungano 22. Usijali na usiwe na haraka, tutazijua hizo serikali mbili au hivyo vyombo viwili na pia hayo mambo ya muungano. Cha kujihakikishia hakikisha unafollow na kusubscribe kupata maarifa haya muhimu yanayohusiana na sheria. @Legal_and_Society