У нас вы можете посмотреть бесплатно NDEGE IKIANGUKA UWANJA WA NDEGE ZANZIBAR, ZAA YAJIPIMA UFANISI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) imefanya zoezi la utayari ikiwa ni sehemu ya majukumu yake ya kawaida ya usalama wa anga, kwa lengo la kupima uwezo wa kukabiliana na matukio ya dharura yanayoweza kutokea katika viwanja vya ndege. Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma ZAA, Mulhat Yussuf Said, amesema zoezi hilo hulenga kupima ufanisi wa mifumo ya dharura, uwezo wa watendaji wa sekta ya anga pamoja na kuimarisha uratibu kati ya taasisi na wadau wa ulinzi, usalama na afya. Ameeleza kuwa mazoezi hayo hufanyika kwa mujibu wa miongozo ya kitaifa na kimataifa ili kuhakikisha viwango vya ulinzi na uendeshaji wa viwanja vya ndege vinazingatiwa ipasavyo, sambamba na kubaini changamoto na maeneo yanayohitaji maboresho. Kwa upande wake, Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume, Amani Hamduni Zuberi, amesema zoezi hilo ni sehemu ya kutekeleza matakwa ya viwango vya kimataifa vya viwanja vya ndege. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar, Makame Hatibu Makame, amesema zoezi hilo limeongeza uelewa wa vitendo kuhusu kiwango cha utayari wa kukabiliana na maafa. #AsamOnlineTV #ZAA #UsalamaWaAnga #ViwanjaVyaNdege #Zanzibar #Utayari #Maafa