У нас вы можете посмотреть бесплатно MSIKILIZE MBUNGE GETERE NA MAJIBU YA SERIKALI KUHUSU PESA YA KIFUTA JASHO NA MACHOZI-JIMBO LA BUNDA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu malipo ya kifuta jasho na machozi kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda waliokumbwa na changamoto ya wanyama wakali, hususan tembo, wanaoharibu mazao. Ufafanuzi huo umetolewa kufuatia swali la Mbunge wa Jimbo la Bunda, Mheshimiwa Buniface Getere, aliyeuliza ni lini wananchi ambao mazao yao yameharibiwa na tembo katika vijiji mbalimbali vya jimbo hilo watalipwa kifuta jasho. Swali hilo limeulizwa leo tarehe 28 Januari 2026 katika Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkutano wa Pili, Kikao cha Pili. Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025, wizara imelipa kifuta jasho na machozi jumla ya shilingi milioni 312,360,000 kwa wananchi 1,115 wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda. Aidha, amesema wizara imekamilisha uchambuzi wa madai mengine ya kifuta jasho na machozi ambapo jumla ya shilingi milioni 524,122,500 zitalipwa kwa wananchi 1,603 wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda. Ameeleza kuwa kwa sasa wizara inakamilisha taratibu za malipo hayo ili wananchi husika walipwe stahiki zao kwa mujibu wa kanuni, kupitia mfumo wa kielektroniki. Hata hivyo, ameongeza kuwa sambamba na matumizi ya mfumo huo mpya, serikali itaendelea kuwalipa wananchi ambao hawana akaunti za benki au namba za simu kwa kutumia utaratibu wa awali, ambapo wataalamu wa serikali hufika moja kwa moja katika maeneo husika kwa ajili ya kufanya malipo.