У нас вы можете посмотреть бесплатно BEI YA UFUTA YALETA UKOMBOZI KWA WAKULIMA. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#knews24 WANANCHI WA KIJIJI CHA MAGAMBA WAISHUKURU SERIKALI KWA KUANZISHA STAKABADHI GHALANI. Wakulima wa Kijiji cha Magamba, Kata ya Magamba Wilayani Songwe mkoa wa Songwe wameishukuru serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe kwa kuanzisha mfumo wa uuzaji wa zao la ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ambao wameutaja kuwa mkombozi wa kilimo chao. Wakulima hao kwa nyakati tofauti wamezungumza hayo baada ya kumalizika mnada wa tatu wa ufuta Wilayani Songwe huku bei zikiendelea kupaa katika kila mnada kuanzia uliofanyika Mei 5 hadi Jumatano Mei 24, 2023. Bi. Pelegia Boniface Simfukwe, 38, akizungumza kando na ghala la Magamba ambako mnada umefanyika amesema amekuwa akilima ufuta kwa muda mrefu hajawahi kuuza ufuta wake katika bei inayokaribiana na mnada wa Leo [Jumatano Mei 24]. "Tulikuwa tunauza ufuta lakini hii bei ni nzuri kwetu wakulima, mwanzoni bei ilikuwa ikipanda sana inakuwa 2,500 hadi 3,000 lakini sasa tumeuza 3,678", alisema Bi. Pelegia akiwa amejifunga kilemba kichwani. Christopher Yunji akizungumza baada ya mnada amesema anaipongeza serikali kwa kuleta mfumo wa stakabadhi ghala ingawa amekiri wazi kwamba mwanzoni alikuwa anahofia lakini sasa amepata uelewa wa namna unavyoendeshwa ataenda kuwahamasisha wakulima wengi zaidi. Pongezi hizo zimetolewa pia na Willy Julius Msukwa ambaye pia ni mkulima wa kijiji cha Magamba ambaye amesema kutokana na mfumo huo anategemea uchumi wa familia yake kuimarika ambapo ameomba serikali kwa mwaka ujao kuanza masoko mapema zaidi. Mnada wa Leo Jumatano, ghala la Magamba ni wa tatu kwa Songwe DC katika mkoa wa Songwe ambapo takribani tani 1555.773 sawa na kilo 1,555,773 zimeuzwa kwa shilingi 3,678. #wizarayakilimo #stakabadhighalani