У нас вы можете посмотреть бесплатно MAFUNZO YA UELEWA KUHUSU HIFADHI YA MJI MKONGWE YAFANYIKA FORODHANI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mafunzo ya uelewa kuhusu hifadhi ya Mji Mkongwe na uhifadhi wa majengo ya kale yalifanyika tarehe 3 Februari 2025 katika eneo la Forodhani, yakiratibiwa na Taasisi ya Mji Mkongwe kwa kushirikiana na Kawa Training Center. Mafunzo hayo yaliwakutanisha wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali, yakiwa na lengo la kuwajengea uelewa juu ya umuhimu wa kulinda urithi wa kihistoria na kitamaduni wa Mji Mkongwe. Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo, Seleh Juma Makame, Afisa Elimu kutoka Mamlaka ya Hifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe, aliwafundisha washiriki umuhimu wa kuhifadhi majengo ya kale pamoja na mbinu sahihi za kuwahudumia na kuwaelekeza watalii wanaotembelea Mji Mkongwe. Kwa upande wake, Bi. Zuhura Ali Juma, ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Makaburi ya Wafalme na Makumbusho, amesema mafunzo kama hayo ni muhimu kwani makumbusho ni sehemu ya jamii, hivyo kuna haja ya wananchi kupewa elimu ili kuongeza muamko wa kutembelea makumbusho na kuthamini historia yao. Amesisitiza kuwa uelewa wa jamii juu ya makumbusho na maeneo ya kihistoria ni nguzo muhimu katika kulinda na kuendeleza urithi wa Taifa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.