У нас вы можете посмотреть бесплатно MHE. HEMED AIPONGEZA NMB KWA IFTARI YA PAMOJA NA WATOTO YATIMA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Alhajj Hemed Suleiman Abdulla, amesema ni jambo la faraja kuona NMB Bank Plc ikiendelea kuwakutanisha wateja wake, wadau na watoto yatima katika Iftari ya pamoja, hatua inayochangia kuimarisha mshikamano na kuleta furaha kwa jamii. Ameyasema hayo baada ya Iftari iliyoandaliwa na benki hiyo katika Ukumbi wa Golden Tulip Zanzibar Airport. Amesema kitendo cha NMB kufuturu pamoja na wateja wake na watoto yatima kinaonesha kuwa benki hiyo si taasisi ya kifedha pekee, bali ni mdau muhimu katika ustawi wa jamii na maendeleo kwa ujumla. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Bank Plc, Bibi Ruth Zaipuna, amesema Iftari hiyo ni sehemu ya kuendeleza mahusiano mema na wadau pamoja na kurejesha shukrani kwa ushirikiano wao. Katika hafla hiyo, Makamu wa Pili wa Rais aliwakabidhi zawadi watoto yatima kutoka Assalaam Orphanage Center na Kidundo Orphanage Center, ikiwa ni ishara ya upendo na kuwajengea furaha watoto hao. #ASAMOnlineTV #NMB #IftariYaPamoja #UstawiWaJamii #Zanzibar