У нас вы можете посмотреть бесплатно WAZIRI SHARIF ARIDHISHWA NA HALI YA BEI ZA BIDHAA UNGUJA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kaimu Waziri wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda ambaye pia ni Waziri wa Kazi na Uwekezaji, Mhe. Sharif Ali Sharif, amesema ameridhishwa na hali ya upatikanaji na bei za bidhaa katika masoko ya Unguja, akibainisha kuwa bei zimeonekana kupungua kwa kiwango kikubwa. Amesema Wizara itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kufuata taratibu za biashara na kuzingatia usafi wa mazingira wanayofanyia shughuli zao. Kauli hiyo ameitoa baada ya kufanya ziara ya kukagua bei za vyakula katika Soko la Darajani, Soko la Mombasa, Soko la Mwanakwerekwe pamoja na Soko la Jumbi. Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara, Ndg. Alya Emanuel Juma, amesema lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha wafanyabiashara wanabandika bei za bidhaa zao ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wananchi. Mkuu wa Soko la Jumbi, Faki Suleiman Hatib, ameeleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili wafanyabiashara ni upotevu wa mitaji, jambo linalohitaji ufumbuzi wa pamoja. #ASAMOnlineTV #BiasharaZanzibar #MasokoYaUnguja #BeiZaBidhaa #UshindaniHalali