У нас вы можете посмотреть бесплатно HOTUBA KAMILI YA RAIS MAGUFULI AKIWA MUSOMA - 05/09/2018 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Rais Magufuli leo tarehe 05 Septemba, 2018 ameendelea na ziara yake katika mkoa wa Mara ambapo amezindua mradi wa maji safi na usafi wa mazingira wa Manispaa ya Musoma, kufungua barabara ya Simiyu/Mara – Musoma na kisha kuhutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja Mukendo Musoma Mjini. Katika hotuba yake Rais Magufuli ameelezea kutoridhishwa na hatua zinazochukuliwa na viongozi wa Wizara, Mkoa wa Mara na vyombo vya dola dhidi ya mfanyabiashara Nyakilang’ani ambaye amelalamikiwa na wananchi wa Mwisenge katika Manispaa ya Musoma kuwa baada ya kuuziwa hoteli ya Musoma amezuia wananchi kukatiza katika eneo hilo wanapotaka kwenda katika mwambao wa ziwa Victoria na hivyo kulazimika kuzunguka umbali mrefu. “Hoteli hii imechukuliwa tangu miaka 10 iliyopita, haijaendelezwa, wananchi wanakosa ajira, Serikali inakosa mapato halafu viongozi mpo mnamuangalia tu, huyohuyo Nyakilang’ani amepewa mradi wa maji wa mji wa Bunda huu mwaka wa 8 na mpaka sasa hautoi maji, viongozi mpo hamchukui hatua. “Sasa nataka hoteli ya Musoma iliyojengwa na Baba wa Taifa kwa nia yake njema ya kuiendeleza Musoma ichukuliwe kwa sababu ameshindwa kuiendeleza” amesisitiza Rais Magufuli. Rais Magufuli pia amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Mara kuwa Serikali itahakikisha inaujenga kwa kiwango cha lami uwanja wa ndege wa Musoma ili uweze kupokea ndege kubwa na ndogo, na kukamilisha ujenzi wa hospitali ya Musoma haraka ili ifanane na hadhi ya hospitali iliyopo katika Mkoa aliozaliwa Baba wa Taifa.