У нас вы можете посмотреть бесплатно KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 10/02/2026 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 10/02/2026 UJUMBE WA LEO: MAMBO YATAKAYOKUWEZESHA KUTOKA NYUMBA YA UTUMWA MPAKA UTIMILIFU WA AHADI Kutoka 20 : 1 - 2 Kutoka 3 : 7 Mwanzo 16 : 13 LENGO LA SOMO 1. Kuelewa Safari ya Ukombozi na namna udhihirisho wa mkono wa MUNGU kuingilia kati hali za watu wake waliopo kwenye nyumba ya utumwa. 2. Nafasi ya Agano la urithi na mauti kutoka kwenye madhara yake ili kunufaika kwa kutoka katika nyumba ya Utumwa. 3. Kujua dalili ya vita inayolenga kipawa chako, ili kubakia utumwani kama lengo la Adui kisitumike kukutoa Utumwani. Kutoka 20 : 1 - 2 1 Mungu akanena maneno haya yote akasema, 2 Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Kutoka 3 : 7 7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; Mwanzo 16 : 13 13 Akaliita jina la Bwana aliyesema naye, Wewe U Mungu uonaye, kwani alisema, Hata hapa nimemwona yeye anionaye? SAFARI YA UKOMBOZI INA HATUA TATU. 1. Mungu anaona utumwa. 2. Mungu anaingilia kwa mkono wake 3. Mungu anatimiza ahadi yake kwa wakati wake. 1. Mungu anatambua hali ya mateso na vifungo vya watu wake. Kutoka 3 : 7 “Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri…” Hakuna mateso yaliyo fichika mbele za Mungu. Hakuna kifungo kinachomshinda Mungu kukitambua. Utumwa wako haupuuzwi wala kusahaulika. Mungu anaona maumivu, dhuluma, machozi, na ukandamizaji. Ni jina la Mungu katika Biblia lenye maana nzito sana kiroho. El Roi maana yake ni; “Mungu anayeona” au “Mungu anayeniona.” Ni Mungu ambaye haoni kwa jumla tu, bali anamuona mtu binafsi, hali yake, maumivu yake, na kilio chake. Mhubiri : Mwl.Renald Mlawi. Kwa maombi na ushauri : Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053 Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga Simu: +255 713 553 443 YouTube: Kijitonyama Lutheran church Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com