У нас вы можете посмотреть бесплатно "MALALAMIKO YA ACT NI MAMBO YA KISIASA SI KISHERIA", ZEC YAIJIBU, ACT YASISITIZA NYARAKA KU... или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#JAMBOTV Chama cha ACT Wazalendo kimeingia kwenye mzozo mzito na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kufuatia mpango wa tume hiyo kuteketeza nyaraka zote za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, hatua ambayo upinzani umeitaja kama jaribio la kuharibu ushahidi wa kesi zilizopo mahakamani. Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho Vuga siku ya Jumatano, Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Ismail Jussa, amesema kuwa kuanzia Januari 21, 2026, chama hicho kilishawasilisha maombi ya kisheria mahakamani ili nyaraka hizo zihifadhiwe kama ushahidi kwa ajili ya kesi 25 za wagombea uwakilishi. Jussa amesisitiza kuwa kuteketeza nyaraka wakati kesi zinaendelea ni "kosa la jinai". Hata hivyo, Mwenyekiti wa ZEC, Jaji George Joseph Kazi akijibu hoja za Jussa, amesisitiza kuwa sheria inawataka kuteketeza nyaraka baada ya siku 90 tangu uchaguzi kukamilika. Amebainisha kuwa kwa sababu hakuna zuio rasmi la mahakama lililowasilishwa kwao, tume itaendelea na zoezi hilo kwa mujibu wa sheria. Ismail Jussa anadai ZEC "inajificha" chini ya Kifungu cha 98(3) cha Sheria ya Uchaguzi Namba 4 ya Mwaka 2018 huku ikijua fika kuwa kuna mashauri ya kisheria yanayohitaji nyaraka hizo kama ushahidi wa msingi. Makamu Mwenyekiti Jussa ametoa wito kwa mamlaka husika kuhakikisha vifaa na nyaraka hizo zinakaa chini ya ulinzi madhubuti, huku Jaji Kazi akishauri kuwa kama ACT Wazalendo wana malalamiko, walipaswa kufuata mkondo wa mahakama kupata zuio rasmi la kisheria kabla ya muda wa siku 90 uliowekwa na sheria haujamalizika. ........... Tufuatilie kwenye mitandao ya kijamii ►YOUTUBE: / @jambotv908 ►INSTAGRAM: / jambotv ►TWITTER: / jambotv_ ►FACEBOOK: / jambotv ►WEBSITE: https://jambo.tz/