У нас вы можете посмотреть бесплатно #JAMBO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
RC MAKALLA ATANGAZA RASMI KAMPENI YA BIMA AFYA MKOA ARUSHA Ataka hamasa ya Bima ya afya kuwa Ajenda ya kudumu kuanzia Ngazi ya Kitongoji Mpaka Mkoa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe.CPA Amos Gabriel Makalla ametangaza kuanza kwa kampeni ya wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya kwa wote katika mkoa wa Arusha, mara baada ya kuzindua zoezi hilo kwa kaya masikini ambazo zimetambuliwa na Serikali. Mhe.Makalla amesema hayo, wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo Februari 04, 2026 na kuwakutanisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya, Wenyeviti, Wakurugenzi na Waganga Wakuu wa Halmashauri pamoja na Maafisa Tarafa wote wa mkoa huo. Amewataka viongozi hao, kufanya Mpango wa serikali wa Bima ya Afya kuwa agenda ya kudumu kwenye maeneo yao kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata, Tarafa, Halmashauri na Wilaya zao na hatimaye kuwasilisha taarifa hizo kwenye mikutano ya mabaraza ya madiwani. "Viongozi wote hakikisheni uhamasishaji iwe ajenda ya kudumu ili wananchi watumie fursa hiyo kujiunga na Bima ya Afya kwa gharama ya shilingi 150,000 kwa mwaka kwa kaya ya watu 6. Waelezeni kuwa Bima hii ya afya itawahakikishia kupata matibabu pindi watakapougua". Amesema Mhe. Makalla Hata hivyo, Meneja wa Bima ya Afya NHIF Mkoa wa Arusha, Hipoliti Lelo, amebainisha kuwa tayari zoezi la uandikishwaji wa kaya maskini limeanza katika jiji la Arusha na litaendelea kwa Halmashauri zote 7 huku jumla ya kaya masikini 12, 741 na walengwa 56,693 wakitarajiwa kuandikishwa na kupatiwa kadi katika awamu hii ya kwanza ya mpango huo wa bima ya afya kwa wote.