У нас вы можете посмотреть бесплатно Wafanyabiashara Mashine Tatu Waomba Msaada wa Rais Samia Baada ya Moto Kuteketeza Soko или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Iringa. Wafanyabiashara wa soko la Mashine Tatu, waliopoteza mali na bidhaa zao kufuatia janga la moto lililotokea hivi karibuni, wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan awasaidie kurejea katika hali zao za kawaida. Wakizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, wafanyabiashara hao walieleza kuwa zaidi ya vibanda 86 viliteketea kwa moto, na kuwacha zaidi ya wafanyabiashara 535 wakiwa hawana pa kuanzia tena maisha yao ya kujitafutia kipato. Akizungumza katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa aliwapa pole waathirika wa janga hilo na kuwahakikishia kuwa serikali iko pamoja nao katika kipindi hiki kigumu. Alisema jitihada zinaendelea kufanyika kwa kushirikiana na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ambalo ndilo mmiliki wa eneo hilo, ili kuhakikisha soko hilo linarejeshwa katika hali yake. “Tunaangalia namna bora ya kukarabati eneo hili na kuwasaidia wafanyabiashara hawa kurejea kazini. Serikali iko pamoja nanyi,” alisema Kheri James. Kwa upande wake, Mwanasheria Moses Ambindilwe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria wa Kujitegemea (TLS) mkoa wa Iringa, aliwapa pole waathirika na kuwatia moyo. Alibainisha kuwa sheria ya mikataba ya mikopo inaruhusu wahusika kuomba kusogeza mbele au kusamehewa muda wa ulipaji wa mikopo, hasa katika nyakati ngumu kama hizi, ili kuwapa nafasi waathirika kujipanga upya.